I want to donate

Sponsor a Child

Facebook Feed

WIMBO HUU UMETUNGWA NA KULETWA KWENU NA MR. B.A. Daudi (a.k.a The King)

TITLE: STOP STIGMA

VERSE 1

Imekua kama hakuna magonjwa mengine
Na ambayo yanatisha zaidi ya UKIMWI
Mbona yapo mengi na sio tu UKIMWI?
Ukimuona mtu kachonga eti ni UKIMWI
Homa za mara kwa mara eti kisha kanyaga miwaya
Kuhara sana na kubanja eti ana miwaya
Mbona mawazo potofu kuhusu janga la UKIMWI?

CHORUS
Nivyema tuendelee, kuonyesha
Upendo zaidi, kwa walio athirika na UKIMWI

VERSE 2

Wengi kati yetu hapa wameathirika
Nawengine hata hawana uhakika
Kama unabisha hauja athirika
Nenda ukapime uli uwe na uhakika
Lakini angalia nawe usije umbuka
Mbona waogopa kupima kama huja athirika?
Ya nini kutubeza sasa sisi waathirika?
Mwenyewe hujapima na hujui kama umeathirika
Kwani jamani mambo yameharibika
Wengine wadai hawataki kuishi kwa presha
Bora upime ndipo uondoe hiyo presha
Nakisha upange mikakati yako juu ya maisha
...

View on Facebook

I want to donate